Timu ya Taifa ya Argentina imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Austria katika mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia 2026.
Katika mchezo huo, mabao yote mawili yalifungwa na Lionel Messi, na kuipatia timu yake pointi tatu muhimu. Ushindi huo umeifanya Argentina kufikisha pointi sita katika Kundi J na kufuzu hatua ya timu 32 bora ya michuano hiyo.
Bao hizo za Lionel Messi zimemwezesha kuandika rekodi mpya ya kuwa mfungaji bora wa muda wote katika historia ya Kombe la Dunia, baada ya kufikisha mabao 18 na kumpiku Mjerumani, Miroslav Klose, ambaye alikuwa akishikilia rekodi hiyo kwa mabao 16.
