Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Ndugu Stephen Wasira, amewasili leo mkoani Kilimanjaro kwa ziara rasmi ya kikazi ya siku 5 Mkoani humo.
Ndg Wasira amepokelewa na viongozi mbalimbali wa chama wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Ndugu Patrick Boisafi, alipowasili Katika Ofisi za CCM Mkoani hapo
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, Ndugu Wasira anatarajiwa kukutana na kuzungumza na viongozi na wanachama wa CCM ngazi zote ndani ya mkoa huo. Lengo ni kuimarisha mshikamano na kupata uelewa wa changamoto zinazowakabili.
Kilele cha ziara hiyo kitakuwa tarehe 8 Juni, 2026 ambapo anatarajiwa kuongoza mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Same.

