Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans SC, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa leo, Mei 25, 2026, kwenye KMC Complex uliopo Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga SC yalifungwa na Duke Abuya pamoja na Allan Okello aliyefunga mabao mawili, huku bao la Namungo FC likifungwa na Hassan Kabunda.
Kufuatia matokeo hayo, Yanga SC imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 60, huku watani wao Simba SC wakishuka hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi 58.
Timu zote zimecheza michezo 25, zikibakiwa na michezo mitano kabla ya kumalizika kwa msimu wa ligi unaoendelea kuwa na ushindani mkubwa.
