Mabingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB, Young Africans S.C. wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe hilo baada ya kuichapa JKT Tanzania mabao 2-0 katika mchezo robo fainali uliopigwa leo, Mei 16, 2026, kwenye Uwanja wa Meja I’llJenerali Isamuhyo.

Mabao ya Yanga yamefungwa kipindi Cha kwanza na Hassa Twalib Wahabi pamoja na Mudathir Yahya AbassiĀ 

Yanga inamsubiri mshindi wa kesho wa mchezo wa robo fainali kati ya Mashujaa na Azam FC ambapo mshindi atacheza na Yanga nusu fainali.