Na. Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Bungeni Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Wizara ilizindua programu ya maandalizi ya kuwanoa watoa huduma za utalii na kuwajengea uwezo wadau waliopo katika mnyororo wa thamani wa utalii.
Akiwasilisha bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Leo Mei 15, 2026, amebainisha kuwa katika awamu ya kwanza waongoza watalii 2,228 wamepatiwa mafunzo ya kuboresha huduma huku programu hiyo ikiendelea katika maeneo mengine ya kimkakati yatakayopokea wageni kwa kuzingatia fursa za ugeni huo.
Pia ameongeza kuwa Wizara itashirikiana na wadau wa sekta binafsi kuandaa vifurushi vya safari kwa washiriki wa AFCON 2027 vitakavyofungamanisha mazao ya utalii na huduma muhimu ikiwemo usafiri, malazi na chakula.
