Na. Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Bungeni Dodoma 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Wizara itatumia watu maarufu na wenye ushawishi mkubwa duniani wakiwemo wanamichezo ili kuongeza hamasa ya kuitangaza Tanzania kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha, amebainisha kuwa watu hao watatembelea maeneo yenye vivutio vya utalii ambapo maudhui mbalimbali yatakayolenga kuitangaza Tanzania yatarekodiwa na kurushwa kupitia tovuti mbalimbali pamoja na mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram, LinkedIn, TikTok, Facebook na mtandao wa X.

Ameyabainisha hayo Mei 15, 2026 Bungeni Dodoma wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Pia ameongeza kuwa mashindano ya AFCON 2027 yanatarajiwa kuwa na watazamaji wa viwanjani milioni 1.8 na wafuatiliaji katika televisheni bilioni 1.9 kupitia vituo vya utangazaji zaidi ya 185 duniani.