Na. Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Bungeni Dodoma 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Wizara imeandaa mkakati wa kuitangaza Tanzania kama kivutio cha kipekee cha utalii kuelekea mashindano ya AFCON 2027.

Aidha, amebainisha kuwa kabla ya mashindano hayo Tanzania itaanza kujitangaza wakati wa Mashindano ya Dunia ya Mpira wa Miguu ya FIFA World Cup yatakayofanyika nchini Marekani kati ya mwezi Juni na Julai mwaka 2026.

Ameyabainisha hayo Mei 15, 2026 Bungeni Dodoma wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Pia ameongeza kuwa Tanzania itashirikisha wadau muhimu wakiwemo watangazaji mashuhuri wa michezo duniani pamoja na kujitangaza kupitia mabango ya kidijitali “billboards” yatakayowekwa katika maeneo ya kimkakati nchini Marekani.