Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Alhaj Hemed Suleiman Abdulla, ameongoza zoezi la upandaji miti katika Hospitali ya Wilaya ya Mvomero leo tarehe 26/04/2026, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Katika tukio hilo, jumla ya miche 100 ya miti ya aina mbalimbali kwa ajili ya kivuli na matunda imepandwa, hatua inayolenga kuboresha mazingira na ustawi wa jamii.
Zoezi hilo liliratibiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Naibu Waziri TAMISEMI, viongozi wa taasisi mbalimbali, wananchi na wadau wa uhifadhi.





