Na Sixmund Begashe, Njombe
Timu ya Maliasili Sports Club ya Pool Table wanaume imewachachafya wapinzani wake katika Michezo ya Mei Mosi Mkoani Njombe hali iliyopelekea kujichotea mashabiki lukuki wa mchezo huo.
Mchezaji wa timu hiyo Bw. Agastony Kayugwa chini ya Makocha wake wachezaji Bw. Robert Mtuya na Shedrack Chugwa, alionesha umairi wakutosha katika kuilenga mipiri hali iliyopelekea kushinda michezo 4 Iliyompeleka robo fainali ambapo alionesha upinzani mkali kwa wababe wenzake.
Akizungumzia mapambano katika Michezo hiyo Bw. Jumanne Ambwene mkazi wa Makete amesema pamoja na uzuri wa wachezaji wengine lakini Maliasili imeonesha umahiri mkubwa kutokana kuwashambulia wapinzani kwa kasi na umekini mkubwa.
“Mimi nilikuwa shabiki wa timu nyingine kwa sababu ndugu yangu alikuwa akichezea huko akatolewa mapema hivyo nikaona huyu wa Maliasili ndie napaswa kumshangilia kwa kuwa Mimi ni Mkulima wa Miti na Maliasili ndio Wizara yetu” alisema Bw. Ambwene
Ushiriki katika Michezo ya Mei Mosi 2026 Mkoani Njombe, pamoja na kuleta mshikamano wa kitaifa, kujenga udugu, kubadilishana maarifa na upendo kwa watumishi wa umma pia uzitangaza shughuli mbalimbali za Wizara na Taasisi husika.




