
Mkurugenzi Mtendaji, Hospitali ya KCMC , Prof. Gilead Masenga (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa TankLink Healthcare Foundation Bw. Siraj Mtulia, Mkurugenzi wa TankLink Healthcare Foundation, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halo Pesa Bw. Magesa Wandwi akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam

………..
Kituo cha Tiba cha Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC), Taasisi ya Shirika la Msamaria Mwema iliyopo Moshi, kwa kushirikiana na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel kupitia huduma ya kifedha ya HaloPesa wametia saini makubaliano ya ushirikiano yatakayowezesha utekelezaji wa miradi ya kijamii yenye lengo la kuokoa maisha ya watanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji, Hospitali ya KCMC , Prof. Gilead Masenga, amesema kuwa lengo ni kushirikiano huo
kuanzisha na kuendesha kampeni ya kitaifa ya uchangishaji fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa (Cardiovascular Centre) katika hospitali ya KCMC.
Prof. Masenga magonjwa yasiyoambukiza yanachangia takribani asilimia 70 ya vifo duniani, huku magonjwa ya moyo na mishipa yakiongoza. Hali hii imeifanya KCMC kuona umuhimu wa kuwekeza katika miundombinu na huduma za kisasa za matibabu ya moyo nchini.
“Huu ni ushirikiano muhimu unaolenga kuleta mabadiliko makubwa katika huduma za matibabu ya moyo nchini. Tunatoa wito kwa Watanzania wote kushiriki katika kampeni hii, kwani kila mchango ni muhimu katika kuokoa maisha.” Prof. Masenga.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa HaloPesa,
Bw. Magesa Wandwi, amesema kuwa HaloPesa, wanatoa jukwaa rahisi na salama kwa watanzania kuchangia kwa urahisi zaidi. Huku akisisitiza kuwa ushirikiano huo unaonesha dhamira ya kutumia teknolojia ya kifedha kuleta mchango chanya katika jamii.
Meneja Masoko HaloPesa, Bi. Aidat Lwiza, amewafahamisha wateja wa Halotel na Watanzania kwa ujumla kutumia huduma ya HaloPesa kuchangia kupitia Lipa Namba 23758475-KCMC MOYO ambapo ameeleza kuwa hakutakuwa na makato kwa wateja wote wa halotel watakaolipa kupitia Lipa namba.
KCMC inatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Halotel, HaloPesa, Tanlink Healthcare Foundation na wadau wote wanaoendelea kuunga mkono juhudi hizi za kuboresha afya na kuokoa maisha ya Watanzania.
Mradi huo umelenga kujenga kituo cha kisasa chenye uwezo wa kutoa huduma kamili za uchunguzi, matibabu na ufuatiliaji wa wagonjwa wa moyo kwa Tanzania na nchi jirani.




