Kikosi Cha Azam FC wamefanikiwa kutoka sare tasa ya bila kufungana dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo, Machi 15, 2026, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Azam FC waliokuwa wenyeji walionekana kumiliki sehemu kubwa ya mchezo kwa kutengeneza mashambulizi mara kwa mara, huku Yanga wakicheza kwa tahadhari zaidi wakijikita katika safu ya ulinzi ili kuzuia hatari kutoka kwa wapinzani wao.

Licha ya jitihada za pande zote mbili, hadi dakika 90 za mchezo huo hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake, hivyo mechi kumalizika kwa sare tasa ya 0-0 na kila timu kujinyakulia pointi moja