***********************
Wakazi wa Kawe Mkwamani wanaokaa pembezoni mwa mto mbezi watakiwa kuacha kuendelea kuchukua mchanga katika mto huo ili kuondokana na uhalibifu wa miundombinu na nyumba zilizopo karibu na mto huo hasa kutokana na kuharibika kwa kingo za mto.
Ameyasema hayo Afisa wa maji Bonde la Wami-Ruvu Mhandisi Simoni Ngonyani alipotembelea eneo hilo na kushuhudia zoezi hilo likiendelea kwa wachimbaji hao.
“Nyumba za watu zinabomoka, watu wanachimba wanaenda hadi kwenye kuta za nyumba na kuanguka, hivyo haiwezekani uchimbaji huo ukiendelea katika eneo hili”. Amesema Mhandisi Ngonyani.
Aidha Mhandisi Ngonyani amesema kuwa sheria za rasilimali za maji ya mwaka 2009 namba 11 mwenye mamlaka ya kutoa vibali kwaajili ya watu kuingia mtoni kwaajili ya shughuli yoyote ile ni bonde hasa wao Wami-Ruvu sio halmashauri kwasasa.
Kwa upande wa Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Kawe ASP. Dkt. Ezekieli Kyogo amewataka wachimbaji wamchanga wa maeneo hayo kufuata sheria na taratibu zilizowekwa ili wasiweze kuingia katika matatizo.
“Kama wanataka kuchimba mchanga wanatakiwa kufuata sheria kwani kila kitu kina utaratibu wake zilizowekwa na kama wakiamua kutofuata sheria basi sheria itachukua mkondo wake”. Amesema ASP. Dkt. Kyogo.