Home Mchanganyiko Ummy Mwalimu ametoa tahadhari kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola

Ummy Mwalimu ametoa tahadhari kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola

0

************************

Na WAMJW- Mwanza

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametoa tahadhari kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ulioripotiwa katika nchi ya demomokrasia ya Kongo na sasa katika nchi jirani ya Uganda.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa Ebola katika kituo kilichotengwa kwa ajili ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo wahisiwa wa Ebola endapo utaingia nchini kilichopo Buswelu wilayani Ilemela.

Waziri Ummy ametoa tahadhari kwa Mikoa yote ya Tanzania, kuchukua hatua stahiki za kujikinga na kudhibiti ugonjwa wa Ebola usiingie nchini kwa kutekeleza baadhi ya mambo ikiwemo, kuepuka kugusa damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi na majimaji mengine yanayotoka Mwilini mwa Mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa wa, Ebola.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa Mkoa wa Mwanza ni moja kati ya mikoa mitatu iko katika hatari zaidi ya kupata Ugonjwa huo, ikifuatiwa mkoa wa Kagera,

Hata hivyo, Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imekwishapeleka jumla ya seti 3,500 za vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa afya kupitia ofisi za kanda za MSD.

Aliendelea kusema kuwa, kutokana na tishio la sasa tutaongeza seti 4,000 na kuzipeleka karibu zaidi na wananchi ikiwa ni pamoja na kwenye hospitali zote za Mikoa na Wilaya kwa ajili ya kujiandaa.

” Kufuatia kuendelea kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini DRC/Kongo ambapo jumla ya wagonjwa 2,108 wamethibitishwa kuwa na ugonjwa huu na vifo 1,411 (sawa na 67%) na kufuatia mlipuko mpya wa ugonjwa huu nchini Uganda (ambapo watu 3 wamethibitishwa kuugua ugonjwa huu kuanzia tarehe 11/6/2019;

Aidha, ametoa Tahadhari kwa Umma kuhusu uwepo wa tishio la Mlipuko wa Ebola nchini kwetu hasa kufuatia kuwepo kwa ugonjwa huu nchini Uganda. Hii ni kutokana na mwingiliano mkubwa wa wananchi na kuwasihi wananchi kutokuwa na hofu kwani mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa hapa nchini.