Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma maandishi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari Mbagwa wilayani Nzega, Machi 13, 2025. Kulia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nassoro Hamdan, wa pili kushoto ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamis Kigwangwala na kushoto ni mbunge mstaafu wa Nzega, Lucas Seleli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Mbagwa, Jimbo la Nzega Vijijini, Machi 13, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wakifurahia hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Mbagwa, Jimbo la Nzega Vijijini, Machi 13, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt, Hamisi Kigwangwala alipotoa salamu katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Mbagwa wilayani Nzega, Machi 13, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na wabunge Selemani Zedi wa Bukene (kulia), Dkt. Hamis Kigwangwala wa Nzega Vijijini (wa pili kulia) na Seif Gulamali wa Manonga baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Shule ya Sekondari Mbagwa wilayani Nzega, Machi 13, 2025. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Cornel Lucas Magembe na watatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)