Na Oscar Assenga, KOROGWE.
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (Tughe) Mkoa wa Tanga wametumia maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani kwa kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa waliopo katika Hospitali ya Afya ya Akili ya Lutindi wilayani Korogwe
Akizungumza mara baada ya kukabidhi misaada hiyo Mwenyekiti wa Tughe Mkoa wa Tanga Best Jerry Mitondwa alisema kwamba huo ni utaratibu wao ambao wamejiwekea kuyafikia makundi mbalimbali yenye uhitaji kwa kuwafariji .
Alisema kwamba wanawashukuru watu wote ambao waliofanikisha kupatikana kwa vitu hivyo huku akieleza kwamba kuna umuhimu wa jamii kuondokana na ukatili wa kijinsia pamoja na mila potofu za ukatili wa kijinsia kwa wakina mama.
Awali akizungumza Makamu wa Kamati za Wanawake wa Tughe Mkoa wa Tanga Mwenuekiti Grace Mrinji alisema wamepeleka mahitaji mbalimbali katika Hospitali hiyo ikiwemo magodoro, mashuka, mablangetu na mahitaji ya vyakula.
“Wanawake ni Jeshi kubwa na tuna kazi kubwa kwenye jamii tunajua kwenye jamii yapo mambo meng ya kikatili yanafanyika lakini wanashindwa na kujua wakayasema wapi hivi sisi tutakuwana kazi kubwa kuhakikisha tunaelimisha jamii kuona namna nzuri ya kuyasema kwenye vvyombo mbalimbali vya kisheria ili kuweza kuyakomesha”Alisema
Naye kwa upande Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Katyetye Marwa alisema hospitali inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya Wagonjwa kutekelezwa na ndugu zao hasa kipindi wanapokuwa wakiwapeleka kushindwa kuwafuatilia na hivyo kuwa mzigo kwa hospitali kuchukua jukumu la kuwatunza jambo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa kwao.
Alisema hospitali hiyo ilianzishwa mwaka 1896na wamisionari wa kijerumani ilianza kama kituo cha kulelea watoto yatima ambao wazazi wao walichukuliwa kupelekwa utumwani na walianza Dar na baadae kukihamishia Bagamoyo na baadhi ya watoto kupata changamoto ya malaria walifariki.
Aidha alisema ilipofika mwaka 1904 waliamua kuanzisha kituo maalumu na walipatikana wagonjwa wawili wa afya ya Akili kutoka kwenye Mashamba ya Mkonge na wazungu walipotoka kutafuta mahitaji waliwachukua na kuwatunza kwenye kituo hicho.
Alisema baadae walipotoa taarifa kwao viongozi wao ujerumani na kuwapa ruhusa ya kuanzia hospitali ya Wagonjwa wa Akili walianza na wagonjwa wawili na kufikia mwaka 1914 idadi ya wagonjwa ilikuwa imeongezeka kufikia 80 kwa hiyo tokea kipindi hicho mpaka leo hii hospitali ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 120 kati yao 90 wanaume na 30 wanawake.
Aidha alisema Hospitali hiyo inamilikiwa kanisa la KKT Dayosisi ya Mashariki kwa ubia na Serikali mpaka sasa wana wagonjwa 146 na hivyo kuwa na ongezeko la wagonjwa 26 kumekuwa na changamoto ongezeko kubwa la wagonjwa wanaohitaji huduma.
“Tunawashukuru Tughe kwa msaada huo ambao wametupatia tunashukuru sana na Mwenyezi Mungu awaongezee pale mlipotoa kwa maana vitu ambavyo mmetupatia vitatusaidia sana “Alisema