Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha;Mhe. Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mhe. Abdallah Hamis Ulega kuwa Waziri wa Ujenzi.
Mhe. Jerry William Silaa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfried Mahundi kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Hamis Mohamed Mwinjuma kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Dkt. James Henry Kilabuko kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Dkt. Stephen Justice Nindi, kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo (anayeshughulikia masuala ya Ushirika na Umwagiliaji), kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha mabalozi wafatao;
Bw. Anderson Gukwi Mutatembwa.
Bw. Mobhare Holmes Matinyi.
CP Hamad Khamis Hamad.
CP Suzan Salome Kaganda
Bw.Thobias Masandiko Makoba, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024.