Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ,Jaji Mstaafu Mhe. Mathew Mwaimu,akizungumza wakati akifunga  maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa kwa mwaka huu,yaliyofanyika leo Disemba 12,2024 jijini Dodoma.

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma  Bw. Mathew Kirama,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa kwa mwaka huu,yaliyofanyika leo Disemba 12,2024 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ,Jaji Mstaafu Mhe. Mathew Mwaimu (hayupo pichani)  wakati akifunga  maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa kwa mwaka huu,yaliyofanyika leo Disemba 12,2024 jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bi.Neema Mwakalyelye,akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ,Jaji Mstaafu Mhe. Mathew Mwaimu (hayupo pichani) mara baada ya kufunga  maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa kwa mwaka huu,yaliyofanyika leo Disemba 12,2024 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ,Jaji Mstaafu Mhe. Mathew Mwaimu.akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga   maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa kwa mwaka huu,yaliyofanyika leo Disemba 12,2024 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

MWENYEKITI wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu,ameitaka Serikali kutokupuuza malalamiko ya Viongozi na wananchi yaliyojitokeza wakati wa michakato na kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27,mwaka huu yatatuliwe ili yasijitokeze tena katika uchaguzi ujao.

Jaji Mstaafu Mwaimu ameyabainisha leo Disemba 12,2024 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu yaliyoongozwa na kauli mbiu ya tumia haki yako ya Kidemokrasia,chagua Viongozi waadilifu wanaozingatia haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa maendeleo ya taifa letu.

Amesema kuwa ameona  kupitia vyombo vya habari kuhusu malamamiko ya wagombea kuenguliwa, na nyinginezo zilizojitokeza wakati wa upigaji kura na matokeo.
“Sisi kama watendaji ambao baadhi yetu tulisimamia uchaguzi huo wa serikali za mitaa tusipuuze malalamiko hayo na tunapaswa kutafakari na kuyafanyia kazi ili changamoto hizo zilizojitokeza katika uchaguzi mkuu  wa mwakani.”
Amesisitiza kuwa “kumekuwa na changamoto ambazo zimetajwa katika vyombo vya habari na wengine wamejitokeza hadharani ninachosema kama viongozi ambao tumeshiriki kusimamia uchaguzi baadhi yetu tusipuuze malalamiko haya tuyafanyie kazi ili kama yapo ya kweli tuondokane nayo katika uchaguzi wa mwakani.”

Katika hatua nyingine Jaji Mstaafu Mwaimu amewaonya watumishi wasiozingatia haki za binadamu wakati wa kutekeleza majukumu yao kwani kanuni za utendaji katika utumishi wa umma zinaeleza kuhusu mienendo na tabia zinazofaa kwa watumishi wa umma.

Amesema  lengo la uwepo wa kanuni hizo ni kuhakikisha watumishi wanatoa huduma zinazokidhi matarajio ya wapokea huduma ambao  wananchi hivyo huduma ikitolewa kwa upendeleo, dharau, dhihaka, chuki, maringo, kejeli anakua amekiuka baadhi ya kanuni.
“Mienendo isiyofaa miongoni mwetu itakwenda kukoma hususani vitendo vya rushwa na uvunjifu wa haki za binadamu, wakati tunapotoa huduma kwa umma. hivyo nawaasa kutumia vizuri kongamano hili ili matokeo yalete ufanisi katika utekelezaji majukumu.”amesisitiza

Kwa upande wake Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma  Bw. Mathew Kirama,amesema Maadhimisho hayo uratibiwa kwa pamoja na taasisi zinazosimamia maadili, mapambano dhidi ya Rushwa na Haki za utawala bora nchini na imeamuliwa watumishi wote wakutane na kutafakari ya ndani kupitia kwenye uwasilishaji wa mada mbalimbali. 

“Kwa hiyo kupitia uwasilishaji wa mada tutaweza kubadilishana mawazo na kujua namna ya kuweza kusaidiana kisha kujadili kwa pamoja na kuimarishana sisi kwa sisi ili kuongeza ufanisi katika kutuo huduma kwa umma,”amesema.

Akitoa neno la shukrani Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Bi.Neema Mwakalyelye,amesema kuwa   watatekeleza majukumu yao kwa kuzangatia maadili na haki za binadamu kuhususani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani.