Katibu Tawala mkoa wa Arusha ,Musa Massaile   akizungumza katika.semina hiyo mkoani Arusha

Mkurugenzi wa uendeshaji  kutoka PSSSF, Mbaruku Magawa akizungumza kwenye semina hiyo .
 
…………
Happy Lazaro, Arusha 
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeandaa semina maalumu ya siku mbili jijini Arusha kwa ajili ya wastaafu watarajiwa ili kuweza kujipanga  mapema kabla hawajastaafu na kuondokana  na changamoto mbalimbali .
Aidha  semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo wa kujiandaa na maisha baada ya kustaafu, ikiwa ni pamoja na uelewa wa uwekezaji wa fedha wanazozipata mara baada ya kustaafu.
Akizungumza wakati wa kufunga semina hiyo, mgeni rasmi Katibu Tawala mkoa wa Arusha ,Musa Massaile  amewataka wastaafu watarajiwa kutumia elimu waliyoipata kwa manufaa yao, kuhakikisha wanakwepa matapeli wa mitandao, na kuendelea kuhifadhi siri za serikali na taasisi mlizozitumikia hata baada ya kustaafu.
Aidha amewataka waajiri kuhakikisha michango ya watumishi wao inawasilishwa kwa wakati kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, huku akisisitiza uzalendo na kuwafundisha vijana maadili kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya Taifa.
“Nawaombeni sana mhakikishe mnaepuka matapeli  wa mitandaoni kwani wapo wengi na kai yao kubwa ni kufanya utapeli  kuweni makini sana na msikilize semina hii kwa makini kwani ina mambo mengi mazuri ambayo yatawasaidia kwa kiwango sana .”amesema.
Aidha amewata kuhakikisha wanafahamu haki zao baada ya kustaafu huku wakihakikisha wanakuwa na  nidhamu ya matumizi ya fedha .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa uendeshaji  kutoka PSSSF, Mbaruku Magawa  amesema kuwa wanaendeleza zoezi lao la kuongea na wastaafu watarajiwa na utaratibu huu wa kuongea na wastaafu  walianza tangu mfuko ulipoanza na hii ni mara ya tatu.
 “kwetu zoezi hili  ni muhimu sana kwani wastaafu kwa taratibu tangu mtumishi anapoajiriwa tayari wanaanza kujipanga na kujiandaa   na kustaafu. “amesema .
Amesema kuwa lengo la mkutano huu ni kukumbushana na kuunganishwa na kupewa zile njia za kupita ndio maana utaona kwenye vikao kama hivi wanakuwa na wadau mbalimbali pamoja watu wa benki,washauri ,wawekezaji pamoja na wadau wa kilimo pamoja  na afya. 
Ameongeza kuwa ,lengo  la mkutano huo ni kuwarahisishia  ili wanapoenda kustaafu wajue wanapita  wapi pamoja na kuwandaa na kuwafanya wapumzike wajue pa kuanzia. 
“Hii ni  mara ya tatu tunatoa elimu hii na zoezi kama hili  tumeshafanya Dodoma, Mwanza,Mbeya na Arusha lakini pia wanafunga zoezi hilo jijini Dar es Salaamu ambapo kauli mbiu katika semina hii ni “Uwekezaji  wenye tija utakupa uhakika wa maisha yako baada ya kustaafu “amesema Magawa .
Amesema kuwa ,wanalenga watu wanaoenda  kustaafu ndani ya miaka miwili na mwitikio ni mkubwa kwani kikubwa wanapewa  elimu kwenye maswala ya fedha na kufungua njia za wastaafu wao wajue wafanye nini wanapofika kwenye kustaaafu hivyo ni vizuri apate ushauri kwa wataalamu wanaojua  zaidi kuhusu maswala hayo.
“Tumeandaa semina hii kwani huko wanapopata ushauri mtaani ndio huko huko kuna watu  hawana kazi za kufanya bali kazi yao ni kusubiri  hela za wastaafu ili waweze kuwatapeli  hayo ndiyo  tunajaribu  kuwaepusha na kuwafanya wayatambue  mapema na waweze kuendelea nayo.”amesema .
Nao baadhi ya washiriki katika mkutano huo wamepongeza kwa semina hiyo kwani italeta  manufaa makubwa kwao namna ya kujipanga wakati wanapoelekea kustaafu na kuondokana na changamoto mbalimbali.


                                
                             