Katibu Tawala mkoa wa Arusha ,Musa Massaile akizungumza katika.semina hiyo mkoani Arusha
Mkurugenzi wa uendeshaji kutoka PSSSF, Mbaruku Magawa akizungumza kwenye semina hiyo .
…………
Happy Lazaro, Arusha
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeandaa semina maalumu ya siku mbili jijini Arusha kwa ajili ya wastaafu watarajiwa ili kuweza kujipanga mapema kabla hawajastaafu na kuondokana na changamoto mbalimbali .
Aidha semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo wa kujiandaa na maisha baada ya kustaafu, ikiwa ni pamoja na uelewa wa uwekezaji wa fedha wanazozipata mara baada ya kustaafu.
Akizungumza wakati wa kufunga semina hiyo, mgeni rasmi Katibu Tawala mkoa wa Arusha ,Musa Massaile amewataka wastaafu watarajiwa kutumia elimu waliyoipata kwa manufaa yao, kuhakikisha wanakwepa matapeli wa mitandao, na kuendelea kuhifadhi siri za serikali na taasisi mlizozitumikia hata baada ya kustaafu.
Aidha amewataka waajiri kuhakikisha michango ya watumishi wao inawasilishwa kwa wakati kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, huku akisisitiza uzalendo na kuwafundisha vijana maadili kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya Taifa.
“Nawaombeni sana mhakikishe mnaepuka matapeli wa mitandaoni kwani wapo wengi na kai yao kubwa ni kufanya utapeli kuweni makini sana na msikilize semina hii kwa makini kwani ina mambo mengi mazuri ambayo yatawasaidia kwa kiwango sana .”amesema.
Aidha amewata kuhakikisha wanafahamu haki zao baada ya kustaafu huku wakihakikisha wanakuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa uendeshaji kutoka PSSSF, Mbaruku Magawa amesema kuwa wanaendeleza zoezi lao la kuongea na wastaafu watarajiwa na utaratibu huu wa kuongea na wastaafu walianza tangu mfuko ulipoanza na hii ni mara ya tatu.
“kwetu zoezi hili ni muhimu sana kwani wastaafu kwa taratibu tangu mtumishi anapoajiriwa tayari wanaanza kujipanga na kujiandaa na kustaafu. “amesema .
Amesema kuwa lengo la mkutano huu ni kukumbushana na kuunganishwa na kupewa zile njia za kupita ndio maana utaona kwenye vikao kama hivi wanakuwa na wadau mbalimbali pamoja watu wa benki,washauri ,wawekezaji pamoja na wadau wa kilimo pamoja na afya.
Ameongeza kuwa ,lengo la mkutano huo ni kuwarahisishia ili wanapoenda kustaafu wajue wanapita wapi pamoja na kuwandaa na kuwafanya wapumzike wajue pa kuanzia.
“Hii ni mara ya tatu tunatoa elimu hii na zoezi kama hili tumeshafanya Dodoma, Mwanza,Mbeya na Arusha lakini pia wanafunga zoezi hilo jijini Dar es Salaamu ambapo kauli mbiu katika semina hii ni “Uwekezaji wenye tija utakupa uhakika wa maisha yako baada ya kustaafu “amesema Magawa .
Amesema kuwa ,wanalenga watu wanaoenda kustaafu ndani ya miaka miwili na mwitikio ni mkubwa kwani kikubwa wanapewa elimu kwenye maswala ya fedha na kufungua njia za wastaafu wao wajue wafanye nini wanapofika kwenye kustaaafu hivyo ni vizuri apate ushauri kwa wataalamu wanaojua zaidi kuhusu maswala hayo.
“Tumeandaa semina hii kwani huko wanapopata ushauri mtaani ndio huko huko kuna watu hawana kazi za kufanya bali kazi yao ni kusubiri hela za wastaafu ili waweze kuwatapeli hayo ndiyo tunajaribu kuwaepusha na kuwafanya wayatambue mapema na waweze kuendelea nayo.”amesema .
Nao baadhi ya washiriki katika mkutano huo wamepongeza kwa semina hiyo kwani italeta manufaa makubwa kwao namna ya kujipanga wakati wanapoelekea kustaafu na kuondokana na changamoto mbalimbali.