Katibu Mkuu wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto), akizungumza na Watumishi wa Wizara yake, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Kingu amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na kujituma zaidi kwa mwaka mpya wa 2020. Aliyevaa tai ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima.
Katibu Mkuu wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto), akizungumza na Watumishi wa Wizara yake, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kingu amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na kujituma zaidi kwa mwaka mpya wa 2020. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima, na kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Emmanuel Kayuni.
Katibu Mkuu wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Wizara hiyo, Emmanuel Kayuni, alipokuwa akifafanua jambo katika kikao cha Watumishi kilichofanyika, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Meja Jenerali Kingu amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na kujituma zaidi kwa mwaka mpya wa 2020. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima.
Katibu Mkuu wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (katikati), akizungumza na Watumishi wa Wizara yake, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Kingu amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na kujituma zaidi kwa mwaka mpya wa 2020.
Katibu Mkuu wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (katikati), akizungumza na Watumishi wa Wizara yake, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Kingu amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na kujituma zaidi kwa mwaka mpya wa 2020. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
………………..
Na Mwandishi Wetu, MOHA, Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, amewataka Watumishi wa Wizara yake kufanya kazi kwa ushirikiano na kujituma zaidi kwa mwaka mpya wa 2020.
Meja Jenerali Kingu ameyazungumza hayo katika kikao na watumishi wa Wizara hiyo, kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo, ambacho kikao hicho kililenga kutoa salamu za mwaka mpya wa 2020 na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa kasi ndani ya mwaka huu.
“Lengo la kikao kikao hiki ni kupeana salamu za mwaka mpya, na pia tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kutufikisha mwaka huu salama, wengi hawakufika lakini mimi na wewe tumefika, hivyo tuendelea kufanya kazi kwa upendo,” alisema Kingu.
Aliongeza kuwa, Mwaka 2020 ni mwaka wa kazi na ushirikiano, licha ya kuendelea kufanya majukumu yetu lakini watumishi wawe wazi katika masuala yote ya kazi ili kuleta ufanisi na mafaniko ndani ya Wizara hiyo.
“Mwaka huu tunapaswa tubadilike zaidi, tufanye kazi, kila mtu awajibike kutokana na kazi anazozifanya, Mungu atupe uzima na afya, tuwe na umoja, upendo katika kutekeleza wajibu wetu kisawasawa, na atakayefanya kazi atapewa haki yake na siyo kuishi kiujanjaujanja,” alisema Kingu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu (DAHRM), Emmanuel Kayuni, alimshukuru Katibu Mkuu kwa kikao hicho, na kuwataka watumishi kufuata maagizo yake na pia kuendelea kufanya kazi kwa umoja na kutii sheria za kazi.