Wakiwa ugenini katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma wachezaji wa Wekundu wa Msimbazi Simba Sc na benchi la ufundi baada ya dakika 90 kumalizika wamefanikiwa kupata ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya Dodoma Jiji.
Bao pekee la ushindi limefungwa na Jean Ahoa dakika ya 63 kwa pigo la penalti baada ya mwamuzi kuamuru ipigwe penalty baada ya kutafsri kuwa nahodha wa Simba SC Mohamed Hussen Zimbwe Jr alikuwa amechezewa faulo ndani ya 18.
Ni bao la pili Ahoa anafunga katika ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/25 huku Simba Sc ikifikisha poini 12 baada ya kucheza michezo nne ya Ligi Kuu ya Tanzania bara na kushinda zote.