Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe. Said Juma Mshana amekutana na Waziri Mkuu wa DRC, Mhe. Judith Simunwa Tuluka jijini Kinshasa Septemba 11, 2024. Mhe. Mshana kwa niaba ya Serikali ya Tanzania alitumia fursa hiyo kuwasilisha salamu za pongezi kwa Mhe. Waziri Mkuu kwa kuaminiwa na kuteuliwa na Rais wa nchi hiyo, Mhe. Felix Antoine Tshisekedi kushika wadhifa huo muhimu katika Serikali ya DRC..