Tanzania inashiriki Kongamano na Maonesho ya Kimataifa ya Viwanda vya Dawa, Vifaa Tiba, Chanjo na Vitendanishi (CPHI) yanayofanyika Milan, Italia, tarehe 6–8 Oktoba 2026.

Ushiriki huo umefungua fursa muhimu kwa Tanzania kukutana na wawekezaji na wadau wakubwa wa sekta ya bidhaa tiba duniani, kwa lengo la kuvutia uwekezaji na kuendeleza uzalishaji wa bidhaa tiba nchini.

Chini ya mwavuli wa Kikosi Kazi cha Kuharakisha uanzishaji wa viwanda tiba nchini (PIAT), ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara wa Afya, Bw. Emmanuel Tayari, anayeshiriki katika majadiliano na wadau mbalimbali kuhusu fursa za ubia na uwekezaji katika viwanda vya bidhaa tiba.

Hatua hii inaunga mkono utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 kwa kuongeza uzalishaji wa ndani na kupunguza utegemezi wa bidhaa tiba kutoka nje, sambamba na kuimarisha upatikanaji wa bidhaa tiba bora na salama kwa afya ya jamii.