Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa kituo cha mazoezi na kupumzikia Jijini Dodoma, kampuni ya Beijing Construction Engeneering Group (BECG) aongeze kasi ya ujenzi kwa kufanya kazi usiku na mchana ili kituo hicho kiweze kukamilika na kuanza kutumiwa na wananchi.
Katibu Mkuu Msigwa ametoa kauli hiyo leo Julai 30, 2024 alipotembelea eneo la ujenzi wa Kituo hicho Nanenane Jijini Dodoma na kushuhudia baadhi ya kazi zikiwa zinaendelea huku ujenzi huo ukiwa umefikia asilimia 53 ukihusisha viwanja vya michezo mbalimbali, mabwawa ya kuogelea jengo la utawala, vyumba vya wachezaji na majukwaa ya watazamaji.