Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe George Simbachawene akizungumza na Mawakili wakati wa ufunguzi wa Mafunzo maalamu kwa Mawakili wa Serikali yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jijini Dodoma hivi karibuni
……………………
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliratibu na kuendesha mafunzo kwa Mawakili wa Serikali.
Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo Mawakili kwenye masuala mbalimbali yanayohusu sheria ikiwemo Uandishi wa sheria, mambo muhimu ya kuzingatia kwenye Mikataba na Makubaliano baina ya Nchi au Taasisi, pamoja na mambo ya kuzingatia katika kuishauri Serikali kwenye nyanja ya Sheria.
Mafunzo hayo yalifanyika Jijini Dodoma hivi karibuni na kuhudhuriwa na Mawakili takribani mia mbili na tisini (290) kutoka taasisi mbalimbali za Serikali.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akizungumza wakati wa mafunzo kwa Mawakili wa Serikali yaliyoandaliwa na kuratibiwa na Ofisi hiyo Jijini Dodoma
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Balozi Prof. Kennedy G. Gastorn akifafanua jambo wakati wa Semina na Mafunzo kwa Mawakili kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali yaliyofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Balozi Prof. Kennedy G. Gastorn akifafanua jambo wakati wa Semina na Mafunzo kwa Mawakili kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali yaliyofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni
Sehemu ya wakufunzi wa mafunzo kwa Mawakili wa Serikali wakifuatilia kwa ukaribu mada mbalimbali zilizotolewa kwenye mafunzo hayo
Baadhi ya Mawakili wa Serikali wakisikiliza hoja na mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mafunzo kwa Mawakili hao yaliyofanyika jijini Dodoma
Mawakili wakifuatilia kwa umakini mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hivi karibuni Jjini Dodoma
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akigawa vyeti kwa Mawakili kutoka Taasisi za Serikali walioshiriki mafunzo kwa Mawakili yaliyofanyika Jijini Dodoma