Walengwa 10 wa mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf manispaa ya Tabora kutoka kikundi cha mkombozi wakiwa katika shamba lao wakivuna mahindi
Mratibu wa TASAF Manispaa ya Tabora Happy Mtutwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya maeneleo ya walengwa wa Tasaf .
Afisa ugani manispaa ya Tabora Happiness Nnko akitoa ufafanuzi juu ya walengwa wa mfuko wa maendeleo Tasaf.
………………
Na Lucas Raphael,Tabora
Walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF katika kata ya Misha manispaa ya Tabora wameishukuru serikali kwa kuwezesha wataalamu wa kilimo kuwafikia kwenye maeneo yao na kuwapatia elimu ya kilimo ambayo imewasaidia kufanya shughuli za kilimo kitaalamu na hivyo kujikwamua kiuchumi.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu kikundi cha Mkombozi Khadija Juma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea wakati wakivuna mahindi katika shamba la kikundi hicho katika kijiji cha Igambilo kata ya Misha Manispaa ya Tabora .
Alisema alisema kwamba serikali kupitia halmashauri ya manispaa ya walipatia pembejeo zote za kilimo ambacho walifanikiwa kulima kisasa na kupata mahindi yakutosha licha ya changamoto ya mvua za masika msimu wa kilimo mwaka huu.
Khadija aliendelea kusema kwamba wanaishukuru TASAF kwa kuwezesha kimaisha hata kuweza kula mila mitatu kwa siku na kufikia hatua ya kuweza kuanzisha kikundi cha kilimo na kulima mazao ya mahaindi na Alizeti kwa lengo la kupata chakula na mafuta ya kupikia.
Alisema kwamba moja ya changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili walengwa hao ni kutofikiwa na maafisa ugani hali ambayo ilisababisha kuendesha shughuli zao za kilimo kwa mazoea.
Mratibu wa TASAF Manispaa ya Tabora Happy Mtutwa alisema kwamba halmashauri ya manispaa Tabora ina jumla ya vikundi kuweka na kukopa 149 vilivyosajiliwa kwa ajili ya kuwezesha walengwa na mfuko huo.
Alisema kwamba vikundi hivyo vya kuweka na kukopa vinamtaji wa zaidi ya shilingi milioni 25 lengo ni kusaidiana wao kwa wao ikiwa ni njia ya kuwanyua kiuchumi.
Alisema kwamba kuna baadhi ya vikundi viliunganishwa na maafisa ugani wa kata husika ili waweze kufanya shughuli za pamoja za kilimo .
Afisa ugani manispaa ya Tabora Happiness Nnko alisema kwamba hatua hiyo imerejesha matumaini mapya kwa walengwa wa mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf wanaoendesha shughuli za kilimo ili kujikwamua kutoka kwenye umasikini,
Alisema wanaishukuru serikali kwa kuwezesha tasaf kuanzisha mpango wa kuazisha vikundi vya kuweka na kukopa katika msimu huu wa kilimo 23/24 kuwezesha kuanzisha shughuli za kilimo ambapo waliweza kulima kwa kufuata maelekezo na kufanikiwa kupata mazao yaliyobora .
Alisema elimu waliyotoa juu ya kilimo kwa walengwa hao itasaidia hata kipindi kijacho kwa ajili ya kuendelea kunufaika na mazao hayo.
“Hili ni zoezi la awali ambapo halmashauri ilitoa mbegu,mbolee na wataalam kwa ajili ya kuwasiadia walengwa wa Tasaf mbinu sahihi za kilimo cha kisasa katika heka moja kwa ajili ya majaribio”alisema Happiness