Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega  (kushoto) wakishuhudia  makabidhiano ya Kituo Atamizi cha Ufugaji wa Kibiashara kwa Vijana Kongwa kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI), Profesa Erick Komba (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya PASS TRUST, Yohane Ibrahim Kaduma, Mei 13, 2024. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Shamba la Mifugo Taliri Kongwa mkoani Dodoma. Kulia ni Balozi wa Denmark nchini, Matte Norgaard Dissing-Spandet. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega kuhusu ng’ombe wanaofugwa katika Ranchi ya Kongwa iliyopo Dodoma alipoitembelea, Machi 13, 2024. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama wakati aliposhiriki  tukio la Makabidhiano ya Kituo Atamizi cha Ufugaji wa Kibiashara kwa vijana katika shamba la Mifugo Taliri Kongwa mkoani Dodoma, Mei  13, 2024. Kushoto ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika Mstaafu na Mbunge wa Kongwa , Job Ndugai alipowasili katika Ranchi ya Kongwa mkoani Dodoma kushiriki tukio la Makabidhiano ya Kituo Atamizi cha Ufugaji wa Kibiashara kwa vijana katika shamba la Mifugo Taliri Kongwa mkoani Dodoma, Mei  13, 2024. Katikati ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega kuhusu malisho bora ya ng’ombe alipotembelea Ranchi ya Kongwa mkoani Dodoma, Mei 13, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wazziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi , Uzinduzi na Makabidhiano ya Kituo Atamizi cha Ufugaji wa Kibiashara kwa vijana Kongwa, Mei 13, 2024. Kushoto ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega na kulia ni Balozi wa Denmark nchini, Matte Norgaard Dissing-Spandet. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)