Bw. Lucas Lukaka Mwakilishi wa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kula kwa mbegu za Pamba cha Mount Meru Millers akizungumza na waandishi wa habari katika Bandari ya Musoma leo.
(PICHA NA JOHN BUKUKU -FULLSHANGWEBLOG- MUSOMA)
………………………………………………………..
Bw. Justine Rukaka Mwakilishi wa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kula kwa mbegu za Pamba cha Mount Meru Millers ameishkuru Mamlaka ya Bandari Ziwa Victoria kwa kurejesha huduma za usafirishaji wa mizigo katika Bandari ya Musoma huduma ambayo imewaondolea adha ya kusafirisha malighafi ya kutumia kiwandani hapo na kupunguza gharama za usafiri.
Rukaka ameyasema hayo leo katika Bandari ya Musoma mbele ya waandishi wa habari ambao wapo katika ziara ya kutembelea na kutangaza miradi ya maendeleo ya bandari zilizo katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa.
Rukaka amesema awali walikuwa wakisafirisha mbegu za Pamba kutoka nchini Uganda na kuzipokelea Bandari ya Mwanza Kusini kabla ya Bandari ya Musoma kurejesha huduma za usafirishaji wa mizigo kwa gharama kubwa, kwa sababu ilibidi mara baada ya kupokea mzigo Mwanza wausafirishe tena kwa maroli kutoka Mwanza kwenda Bunda mahali ambapo kiwanda kipo.
Hivyo kwa Bandari ya Musoma kuanza tena huduma za usafirishaji wa mizigo sasa imetupunguzia gharama za usafiri kwa sababu umbali wa Musoma na Bunda siyo mrefu ukilinganisha na Mwanza.
“Tumekuwa tukipokea tani 250 mpaka tani 500 za mbegu za Pamba kwa mara moja kulingana na ukubwa wa meli inayoleta mzigo siku hiyo, hivyo kwetu sisi imekuwa rahisi kwa uendeshaji na uzalishaji wa kiwanda kutokana na gharama za usifiri kupungua”. Amesema Bw. Lucas Lukaka.
Amewaasa wafanyabiashara mbalimbali kutumia bandari ya Musoma kusafirisha mizigo yao ya biashara kwa sababu gharama zake ni za kawaida na unaweza kupakia mzigo kwa wingi tofauti na kusafirisha kwenye maroli.
Kwa upande wa Almachius Vedasto Rwehumbiza Mkuu wa Bandari ya Musoma amesema Bandari hiyo inao uwezo wa kupokea meli tatu kwa wakati mmoja zenye tani 1,500 mpaka 5,000.
“Hivyo nawaasa wafanyabiashara mbalimbali kutumia bandari hiyo ili kufanya biashara kati ya Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda” Ameongeza Rwehumbiza.
Naye Mhandisi wa Bandari za ziwa Victoria Abraham Msina, amesema Ujenzi wa awamu ya kwanza wa Ujenzi wa Gati la Mwigobero bandari ya Musoma umekamilika na tayari limeanza kutumika ambapo limegharimu kiasi cha shilingi milioni 605,036,150.00.
Ameongeza kuwa ujenzi wa miundombinu mingine utaendelea katika awamu ya pili ambao ni jengo la kupumzikia abiria, vyoou majengo mengine ya ofisi na miondo mbinu mingine.
Almachius Vedasto Rwehumbiza Mkuu wa Bandari ya Musoma akizungumza na waandishi wa habari bandarini hapo mara baada ya waandishi hao kutembelea miradi ya maendeleo ya bandari hiyo mjini Musoma leo
Injinia wa Bandari ya ziwa Victoria Abraham Msina akielezea ujenzi kukamilika kwa Ujenzi wa Gati la Mwigobero Bandari ya Musoma Kazi kazi ambayo imekamilika kwa gharama ya shilingi 605,036,150.00.
Gati kubwa la Bandari ya Musoma lenye uwezo wa kupokea meli tatu za mizigo kwa wakati mmoja.
Baadhi ya shehena zinazosafirishwa zikiwa bandarini hapo.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Mwanza Bw. Geoffrey Lwesya akizungumza na waandishi wa habari leo katika bandari ya Musoma ambao wapo katika ziara ya kutembelea na kutangaza miradi ya maendeleo ya bandari zilizo katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa
Baadhi ya waandishi wa habari wakiangalia gati la Mwigobero Bandari ya Musoma wakati walipotembelea mradi huo ambao umekamilika.