Kaimu Meneja wa Bandari ya Mwanza Bw. Geoffrey Lwesya akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Mwanza ambao wapo katika ziara ya kutembelea na kutangaza miradi ya maendeleo ya bandari zilizo katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa
PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWEBLOG-MWANZA
………………………………………………………
Kaimu Meneja wa Bandari ya Mwanza Bw. Geoffrey Lwesya amesema Kufunguka tena kwa njia ya Mwanza hadi Port Bell nchini Uganda na matumizi ya “Tarrif” linganifu tangu mwaka 2018 na kurejea kwa shughuli za usafirishaji wa mizigo katika bandari ya Musoma ni mambo ambayo yamechangia na kupaisha upatikanaji mapato katika bandari ya Mwanza.
Bw. Godfrey Lwesya mesema Mapato yaliyotokana na shughuli za kupakia na kupakua shehena bandarini (cargo handling operations) yameongezeka kwa wastani wa asilimia 54.6 mwaka 2018/19(Julai-Aprili) sawa na Tsh. 1,138.28 billioni ukilinganisha na mwaka 2017/18 na miaka mingine ya nyuma ambapo yalikuwa chini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Mwanza Bw. Lwesya amongeza kuwa Matumizi ya TEHAMA katika makusanyo kwenye bandari za Kemondo, Mwaloni, Kyamkwikwi, Mwanza Kaskazini na Kusini, Isaka, Mwigobero. Bukoba na Mwalo wake wa Nansio kumedhibiti upotevu wa fedha katika ukusanyaji wa mapato jambo ambalo limeleta tija sana bandari Mwanza.
“Jitihada za kushawishi na Kuwarejesha baadhi ya wateja ambao walikuwa wameacha kutumia bandari ya Mwanza South na Musoma na uboreshaji shughuli za usafirishaji katika mashirika ya TRC na MSCL kumezaa matunda hivyo kama tutafanya juhudi zaidi mafanikio yatakuwa ni makubwa”.Ameongeza
Akizungumzia miradi inayoendelea katika bandari mbalimbali kwenye ziwa Victoria Bw. Godfrey Lwesya amesema Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa katika bandari za Mwanza ni ile iliyopitishwa katika mwaka wa fedha 2016/17 au nyuma kidogo.
Ameongeza kuwa miradi hiyo itaendelea kutekelezwa katika mwaka huu wa fedha wa 2017/18 pamoja na miradi mingine mipya ya mwaka huu wa fedha wa 2018/2019 kwa lengo la kuboresha Bandari ya Mwanza na kuleta tija zaidi.
Miongoni mwa miradi ambayo inaendelea ni Mradi wa Ntama Sengerema ujenzi wa gati ambao sasa umefikia 85%. Sehemu ya kazi iliyobakia ni kuezeka jengo la abiria na umaliziaji wa ujenzi wa vyoo pamoja na mnara wa tenki la maji. Mradi huu unategemewa kukamiliki tarehe 4.8.2019 na umegharimu kiasi cha shilingi 2,224,730,287.00.
Ameutaja pia mradi wa Bandari ya Nyamirembe Chato ambao umefikia 40% ya utekelezaji ambapo kazi iliyobaki ni kumalizia ujenzi wa Gati, jengo la abiria, Jengo la mizigo, uzio, vyoo, mnara na tenki la maji , ujenzi wa chumba cha mashine ya umeme pamoja na chumba cha walinzi. Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti na utagharimu kiasi cha shilingi 4,128,875,194.50 huku miradi mingine mingi ikiendelea katika bandari zingine.
Bw. Godfrey Lwesya ameishukuru serikali ya awamu ya 5 chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na wasaidizi wake kwa usimamizi mzuri wa miradi ya serikali pamoja na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za serikali jambo ambalo limeleta nidhamu ya hali ya juu kwa watendaji na kuifanya Bandari Mwanza kufikia malengo hayo.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Mwanza Bw. Geoffrey Lwesya akizizitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Mwanza ambao wapo katika ziara ya kutembelea na kutangaza miradi ya maendeleo ya bandari zilizo katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa kulia ni Bw. Injinia Abraham Msina.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Mwanza Bw. Geoffrey Lwesya akionyesha meli ya MV Umoja ambayo inabeba mabehewa ya treni kwenda Port Bell nchini Uganda kwa waandishi wa habari walioko kwenye ziara ya kutembelea na kutangaza miradi ya maendeleo ya bandari zilizo katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa
Meli ya MV. Umoja ambayo inabeba mabehewa ya treni ya TRC kwenda nchini Uganda.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Mwanza Bw. Geoffrey Lwesya akionyesha jinsi meli ya kubeba mabehewa inavyounganishwa na (Link Span) wakati wa kupakia mabehewa ya treni.
Hapa meli imeunganishwa tayari kwa kupakia mabehewa ya treni.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiangalia moja ya meli za kubebea mabehewa ya treni.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Mwanza Bw. Geoffrey Lwesya akionyesha kifaa maalum Link Span kinachounganisha meli na katika eneo la kupakilia mabehewa ya treni.
Maroli yakipakia mzigo wa mabati kutoka nchini Uganda ambao umewasili leo kwenye bandari ya Mwanza Kusini.
Mabehewa ya Uganda yaliyoleta shehena ya mabati yakisubiri kupakuliwa.
Meli ya abiria ya MV Clarias inayofanya safari zake kati ya Mwanza na Ukerewe kikipakia abiria katika bandari ya Mwanza Kaskazini.
Baadhi ya abiria wakiwa tayari wamepanda kwenye meli ya MV Clarias kuelekea kisiwani Ukerewe.
Meli ya Mv Clarias ikiondoka katika bandari ya Mwanza kusini kuelekea Nansio Ukerewe leo asubuhi.