Na Albano Midelo ,Mbinga 

MKUU wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mheshimiwa Aziza Mangosongo amekabidhi gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) katika kituo cha afya Kindimbachini.

Mangosongo pia amekabidhi madawati 179  pamoja na vifaa vya kujifunzia katika shule za Msingi 10 zilizopo katika Halmashauri  ya Wilaya ya Mbinga.

Hafla Makabidhiano hayo imefanyika katika viunga vya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mangosongo ameutaka uongozi wa shule zilizokabidhiwa madawati na vifaa hivyo kuhakikisha  vinatunzwa vizuri  ili vitumike  kwa muda mrefu.

” Serikali imetuletea vifaa hivi ni jukumu letu kuhakikisha tunavitunza, nitashangaa  kuona vifaa hivi vimeharibiwa utakuwa ni uzembe mkubwa sana” Alisema Mangosongo

Hata hivyo amempongeza Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri  ya Wilaya ya Mbinga Juma Haji  kwa kutekeleza agizo la kutengeneza madawati  ili kukabiliana na  upungufu wa madawati.

Kwa upande wake Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri  ya Wilaya ya Mbinga Juma Haji amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan  kwa kuleta gari la kubebea wagongwa katika kituo cha afya Kata ya Kindimbachini.