Timu ya Afrika Kusini imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Morocco katika mchezo wa raundi ya mwisho ya 16 Bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2023 nchini Ivory Coast.
Bao la kwanza la mechi hiyo lilipatikana katika kipindi cha pili lililofungwa na Evidence Makgopa, ambaye aliiweka Afrika Kusini mbele dakika ya 57, na kuwapa makali kidogo dhidi ya timu ya Morocco ambayo ilionekana kupendwa zaidi.
Katika mechi hiyo Morocco walipata mkwaju wa penati lakini Achraf Hakimi alikosa na kuzima ndoto za timu yake kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe hilo.
Dakika chache baadaye, Afrika Kusini ikafanikiwa kupata bao lao la pili dakika ya 90+5, lililofungwa na Teboho Mokoena, ambaye alikatisha matumaini ya wamorocco kusonga mbeli katika michuano hiyo.
Katika mchezo mwengine timu ya Taifa ya Mali ilifanikiwa kusonga mbele katika michuano ya AFCON 2023 baada kuichapa Burkina Faso mabao 2- 1.