Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametoa shukrani kwa Kamati ya maandalizi ya sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi mwaka huu chini ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Hemed Suleiman Abdullah kwa uratibu mzuri.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na wachezaji, viongozi wa timu ya Mlandege katika hafla ya chakula cha usiku alichowaandaliwa Ikulu Zanzibar tarehe: 22 Januari 2024.
Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameipongeza Kamati ya Mapinduzi Cup chini ya Mbarouk Suleiman Othman pia amewashukuru wadhamini mbalimbali wa mashindano hayo.
Vilevile ameipongeza timu ya Mlandege kuchukua ubingwa wa Kombe la Mapinduzi mara ya pili mfululizo.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amepokea ombi la timu ya Mlandege kuhakikisha wanapatiwa Jengo la Makao makuu ya klabu yao.