KAMPUNI ya michezo ya kubashiri BETIKA, imewasindikiza mabingwa wawili wa kwanza wanaoelekea nchini Ivory Coast, kushuhudia Michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2023), lengo likiwa kuiunga mkono timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ katika michuano hiyo.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jana Jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa Kampuni hiyo, Juvenalius Rugambwa alisema washindi hao walipatikana kupitia kampeni ya ‘Twenzetu Ivory- Coast ki-VIP’ wamegawanywa katika makundi mawili ili watu wapate fursa ya kutazama burudani mbalimbali.
Kundi la kwanza kati ya hao, watatazana mechi ya Morroco dhidi ya Tanzania na kundi la pili watasafiri Januari 20, kutazama mechi kati ya Tanzania dhidi ya Zambia.
Alisema, jumla ya washindi watakuwa 6, na kwa sasa watatangulia washindi wawili na awamu ya pili wataenda wanne.
Pia, alisema BETIKA imegharamia Kila kitu katika promosheni hiyo kwa kushirikiana na kampuni kubwa ya mitandao ya simu ya Tigo kupitia Tigopesa.
“BETIKA pamoja na Tigo inakwenda kusimamisha Abijan na hii ni katika promosheni yetu ya “Twenzetu Ivory -Coast Ki-VIP” alisema.
Kwa upande wake mshindi wa Promosheni hiyo, Elius Simba ambaye ni mkazi wa Kigoma, alisema amepokea kwa furaha ushindi huo na amepata ushirikiano mzuri kutoka kwa BETIKA hadi kufikia kuanza safari yake ya kwenda kushuhudia mechi hiyo.
“Nimepokea kwa furaha sana tangu siku ya kwanza nimetangazwa, ushirikiano ulikua mzuri kati ya BETIKA na mimi hivyo nimejiandaa kwenda kuiunga mkono Stars, nchini Ivory Coast na naamini katika mechi ya kwanza tutatoka na ushindi mnono,” alisema.
Naye mshindi mwingine, Nassib Staphord alisema ushindi huo aliupokea kwa furaha kwa sababu ni kitu ambacho kinakwenda kuweka alama mpya kwenye maisha yake kwani hajawahi kwenda kuangalia mechi ya Afcon Live nchi za nje.
Aliongeza kuwa, wao kama watanzania wanaenda kuongeza nguvu kwa watanzania wengine ambao walitangulia na wanatarajia kurudi wakiwa na ushindi mkubwa.