MFUKO
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umeungana na wadau wa
michezo nchini, kuchangia timu za taifa za Tanzania zinazoshiriki katika
mashindano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo Taifa Stars, ambayo inashiriki michuano
ya AFCON 2023, inayotarajiwa kuanza Januari 13, 2024 nchini Ivory Coast.
Katika
harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya timu hizo, iliyoongozwa na Waziri
Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, kwenye hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es
Salaam, usiku wa kuamkia Januari 11, 2024, PSSSF imenunua kupitia mnada, jezi
ya marehemu Joel Bendera kwa shilingi milioni 11.
Marehemu Bendera alikuwa kocha mzalendo wa kikosi cha Taifa Stars
kilichoshiriki AFCON kwa mara ya kwanza mwaka 1980.
Pichani,
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto), akikabidhi jezi hiyo, kwa Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhandisi Cyprian
Luhemeja (wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba
(watatu kushoto) na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama PSSSF, James Mlowe.