Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya makaazi (kulia) Mzee Ali Haji akimkabidhi hati ya ardhi kwaajili ya ujenzi wa kiwanja cha michezo cha TAYI ALBAMA Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Abdalla Miraji wakati wa utiaji saini hati ya makubaliano ya ujenzi huo, hafla iliyofanyika Ukumbi wa Skuli ya Dkt.Ali Mohammed Shein mjini Unguja.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akifurahia burudani kutoka kwa msanii Abdul nadheef Shaka Hassan (dulizo ) wakati wa utiaji saini ujenzi wa Uwanja wa Michezo TAYI Albama, hafla iliyofanyika Ukumbi wa Skuli ya Dkt.Ali Mohammed Mjini Unguja .
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akizungumza wakati wa utiaji saini ujenzi wa kiwanja cha michezo cha TAYI Albama hafla iliyofanyika Ukumbi wa Skuli ya Dkt sheni Mjini Unguja.
Mwenyekiti wa Taasisi ya TAYI Abdalla Miraji (KULIA)akimkabidhi cheki ya milioni 200 Mwakilishi wa Kampuni ya sky city Abdulrahmani Seleman Said kwaajili ya kuanza ujenzi wa Uwanja wa TAYI Albama mara baada ya kusaini hati za makubaliano ya ujenzi huo huko Skuli ya Dkt.Shein Mjini Unguja.
………………………
Na Sheha Haji Sheha, Maelezo.
Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita ameupongeza Uongozi wa taasisi ya Tanzania Youth Icon (TAYI) kwa mpango wao wa ujenzi wa uwanja wa michezo wa Alabama.
Waziri Tabia ameyasema leo katika hafla ya utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa uwanja huo kati ya Taasisi ya TAYI na kampuni ya Sky City katika ukumbi wa skuli ya Dk. Ali Mohammed Shein Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.
Amesema Uwanja huo utaongeza idadi ya viwanja bora ndani ya Zanzibar ambavyo vitakuwa ni fursa nzuri kwa vijana kukuza vipaji vyao hivyo ni vyema jamii ikatoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuweza kukamilika ujenzi wa uwanja huo kwa wakati.
Naye Mlezi wa TAYI ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amewapongeza wafadhili waliochangia katika kuwezesha mpango wa ujenzi huo kuanza kutekelezwa kwani mradi huo utawasaidia vijana wengi wa Kikwajuni na Zanzibar kwa ujumla katika kuendeleza vipaji vyao.
Mapema Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Youth Icon Abdallah Othman Miraji ameiomba Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwasaidia wataalamu wa kuuendeleza uwanja huo baada ya kukamilika kwake ili uwanja huo uendeshwe kwa ufanisi.
Uwanja huo wa Alabama ambao upo katika Jimbo la Kikwajuni utajengwa kwa muda wa miezi 18 na unarajiwa kutagharimu Shilingi Bilioni 1.7 hadi kukamilika kwake.