Na Brown Jonas – WUSM
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Serikali ya Awamu ya Sita imepanga kujenga uwanja mpya wa Kimatafa wa Gofu katika eneo la Chamwino jijini Dodoma.
Mhe. Dkt. Ndumbaro amesema hayo leo Novemba 23, 2023 Jijini Arusha alipokua akifungua Mashindano ya Kimataifa ya Gofu ya NCBA.
Amesema tayari Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatoa maelekezo juu ya ujenzi wa uwanja huo ambao utachangia kuibua vipaji na kuendeleza Sekta ya michezo hapa nchini.
Mashindano hayo yatafanyika kwa siku nne ambapo wachezaji wa Kimataifa kutoka nchi mbalimbali wanashiriki ikwemo, Tanzania, Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Rwanda, Burundi, Ethiopia na Zambia ambapo zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu kutoka kwa waandaaji zinashindaniwa.