Na Ashrack Miraji Same Kilimanjaro
Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amewaasa vijana kuacha tamaa kuiga tamaduni zisizofaa zilizo kinyume na maadili yaliyo kwenye jamii ikiwemo mchezo mchafu wa kujihusisha katika mapenzi ya Jinsia Moja (Ushoga na Usagaji), biashara haramu ya Dawa za Kulevya Kilimo cha Bangi na Mirungi miongoni mwa viashiria vinavyotajwa kuathiri vijana na kuwa katika hatari ya kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
Ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa mashindano ya michezo ya Dkt.Samia Cup, mashindano yaliyo andaliwa na Mbunge wa jimbo la Same Mashariki Mhe.Anne Kilango akisema uamuzi huo wa Mbunge kuanzisha mashindano utasaidia kuibua vipaji hasa kwa vijana washiriki, pia kuimarisha afya kama inavyo sisitizwa na serikali ikiwa ni miongoni mwa mikakati ya kukabiliana na magonjwa nyemelezi.
“Kipekee nimshukuru sana Mhe.Mbuge sote tunaona kazi kubwa anayoifanya kupambania wananchi kwenye jimbo lake hususani katika kuleta maendeleo hivyo niendelee kutoa rai kwa vijana kushiriki kikamilifu kwenye michezo hii, kwakua itasaidia kupunguza muda wa kukaa vijiweni bila shughuli maalum ambako ndiko mnakutana na vishawishi na kujiingiza kwenye michezo isiyofaa”.amesema mkuu huyo wa Wilaya.
Akifungua michezo hiyo Naibu katibu mkuu Jumuiya ya Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCC) Mussa Peter Mwakitinya amesema Dkt. Samia Cup imekuja ikiwa ni namna ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa iliyofanyika kwenye Jimbo la Same Mashariki ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya Barabara, ujenzi wa madarasa kwenye sekta ya Elimu Msingi na Sekondari pia uboreshwaji wa huduma za afya, n.k, michezo hiyo inalenga pia kukuza vipaji na kujipatia ajira na kuimarisha afya ili kuendelea kuchapa kazi.
“Michezo huondoa mawazo potofu kwa vijana kama wizi na ubakaji kwa mabindi zetu hivyo kama wananchi wa Jimbo la Same Mashariki na vijana kwa Ujumla tumuunge Mkono Mhe.Mbuge kwani anafanya kazi kubwa kwa maslahi ya Jimbo lake na kama mnavyo jionea kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo na kuboresha huduma , jukumu kubwa la Mbunge ni kuweka msukumo kuikumbusha serikali kwenye usimamizi wa Ilani”. Alisema.
“Nitoe pongezi kwa Mhe Mbuge Anne Kilango kwa kuanzisha mashindano haya kwa vijana wa Jimbo la Same Mashariki niimani yangu yatakuwa na tija kubwa kwakuwa wanapo kutana watu tofauti hupata fursa mbalimbali kwa kubadilishana mawazo namna ya kunufaika kupitia shughuli mbalimbali hivyo kuharakisha maendeleo katika jimbo la Same mashariki na Taifa kwa ujumla”.Alisema Mussa Peter Mwakitinyola Naibu katibu Mkuu UVCCM Taifa.