Mbunge wa Jimbo la Ilemela MNEC Mhe Dkt Angeline Mabula ameunga mkono ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza na vitega uchumi vyengine vinavyojengwa katika uwanja wa chama hicho uliopo Capri Point jijini Mwanza kwa kukabidhi mifuko 50 ya Saruji
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mifuko hiyo ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba za watumishi wa CCM mkoa wa Mwanza Mhe Dkt Angeline Mabula amesema kuwa yeye ni Mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Mwanza na ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa hivyo ameamua kuchangia mifuko hiyo ya Saruji kama sehemu ya kuunga mkono ujenzi wa chama chake na kukisaidia kujitegemea kiuchumi
“Tumepokea maombi ya Katibu wa chama kwaajili ya ujenzi wa Nyumba ya mtumishi na mimi nimeguswa nikaamua kuunga mkono kwa kutoa mifuko ya Saruji lakini huu ni mwanzo tutaendelea kushirikiana na naamini wabunge wenzangu nao watajitokeza mara baada ya kuwafungulia njia , “Amesema
Aidha Mhe Dkt Mabula amewataka wanachama na viongozi wengine kuunga mkono ujenzi huo huku akishauri kuongeza vitega uchumi vyengine ili chama hicho kiweze kujitegemea kiuchumi
Kwa upande wake Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Omary Mtuwa mbali na kumshukuru Mbunge huyo Kwa mchango wake ameongeza kuwa ujenzi huo ni utekelezaji wa maagizo ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia halmashauri kuu ya kutaka kujengwa miundombinu na vitega uchumi vya chama nchi nzima
Nae Mhandisi anaesimamia ujenzi huo Bwana Amon Boniphace Malaba amesema kuwa ujenzi huo umefikia asilimia 70 na mpaka mwisho wa mwezi Novemba utakuwa umekamilika