Balozi wa China nchini Tanzania Wang (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali(kushoto)Kamishina Mstaafu wa jeshi la Polisi Suleimani kova(kulia) Naibu wazirI wa maliasili na utalii mhe Constantine John Kanyasu ,waliohudhuria katika kampeni ya kupinga ujangili na utoaji wa misaada iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mhenda wilayani Mvomero.
…………………………………
NA FARIDA SAIDY, MOROGORO
Wananchi wa vijiji wanaoishi karibu na Hifadhi ya Mikumi ikiwemo Kijiji cha Mhenda wametakiwa kuacha kufanya ujangili badala yake kuwekeza zaidi katika Kilimo ili kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo hicho.
Hayo yamesemwa na Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke wakati wa Kampeni ya kuzuia ujangili na kutoa misaada katika Kijiji cha Mhenda wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro yenye thamani ya shiling milioni 1.4 ikiwemo ni pamoja na mbegu za mazao mbalimbali takribani kilo 4800 ili kuweza kuwanufaisha wakazi wa Kijiji hicho kupitia kilimo.
Wang alisema kuwa nchi ya China kwa sasa imeweka adhabu Kali kwa mtu yeyote atakayehusika katika ujangili na hata kukutwa na kosa la ufanyaji wa biashara ya faru na pembe za ndovu kwani soko hilo limefungwa nchini humo kutokan na biashara hiyo kushika kasi huku wanyamaporo wakiendelea kutoweka hivyo ameahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika upingaji ujangili
Awali akipokea misaada hiyo Naibu Waziri waMaliasili na Utalii Costantine Kanyasu huku akiwataka wananchi hao kujikita zaidi katika kilimo kupiti a dhana mbalimbalimbali zilizotolewa na ubalozi wa China ikiwemo mbegu za mahindi katika ulimaji wa tija ili kujipatia kipato na kuachana kabisa na maswala ya ujangili wa wanyama mbalimbali katika hifadhi kwani nchi inategemea kupata zaidi ya watalii Milioni moja watakaotembelea hifadhi ya Taifa hiyo mwaka huu.
Aidha kanyasu ameipongeza Serikali ya China kupitia Ubalozi wake Nchini kwa kuendelea kushirikiana nao hasa katika kuendeleza kilimo kwa kutatua changamoto zinazowakabili katika kilimo hadi kupelekea wakulima kulima kilimo kisicho na tija pia kupinga ujangili kwa kuweka adhabu kali za kisheria juu ya mtu atakayekutwa na makosa ya ujangili wa wanyama pori kutokana na kufungwa kwa soko nchini humo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni isiyo ya kiserikali ya SUKOS KOVA Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleimani Kova alisema ataendelea kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali katika kutatua changamoto mbalimbali zinazokikabili kilimo nchini kwa kuweza kuwasaidia katika utoaji wa vifaa mbalimbali vya kilimo pamoja na kupinga ujangili ili kusaidia utunzaji wa mazingira na wanyamapori.
Pia aliongeza kuwa utoaji wa mbegu katika kijiji cha Mhenda Wilayani Kilosa ni njia moja wapo ya kuwasaidia vijana na wakazi wa kijiji hiko kujikita katika kilimo chenye tija ili kuacha kujihusisha na ujangili hivyo amewataka kuacha kilimo cha mazoea na kulima kilimo cha tija kupitia vifaa mbalimbali ambapo amemuomba balozi kuwanunulia trekta ili wafanye kilimo chenye tija.
Hata hivyo miongoni mwa misaada iliyotolewa katika kijiji cha Mhenda ni pamoja na Mbegu za mahindi kilo 2500, mbegu za alizeti kilo 1500, mbegu za choroko kilo 800, unifomu za ulinzi shirikishi 13, buti za ulinzi shirikishi, komputa mpakato 4 pamoja na runinga 1 ambayo itatumika katika ofisi za TANAPA kwa kuwapa wananchi elimu ya ujangili.