Home Michezo DIWANI WA TENGELEA AMWAGA BAISKEL NA VIFAA VYA MICHEZO.

DIWANI WA TENGELEA AMWAGA BAISKEL NA VIFAA VYA MICHEZO.

0

****************************************

Na Shushu Joel

DIWANI wa kata ya Tengelea,wilaya ya Mkulanga mkoani Pwani Shabani Manda amemwaga baiskeli 11 kwa makatibu tawi wa chama cha mapinduzi (CCM) kwenye kata hiyo kwa lengo la kuwasaidia katika urahisi wa usafiri kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumza na viongozi wa chama hicho diwani Manda alisema kuwa viongozi wa chama wamekuwa wakipata changamoto kubwa ya kuwafikia wanachama kutokana na kukosekana kwa usafiri wa haraka hivyo baiskeli hizi zitasaidia sana.

“Baiskeli hizi naamini zitakuwa suluhisho la viongozi wa ccm kuangaika kuwafikia wanachama wake na hivyo kazi zao zitakuwa nyepesi”Alisema

Aliongeza kuwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa sidhani kama Kuna wapinzani watakao jitokeza kugombea maana utekelwzaji wa ilani ya ccm umefanyika kwa 100%.

Pia diwani huyo amegawa vifaa vya michezo vya mpira wa miguu kwa timu 20 kutoka kila kitongoji.

Aidha aliongeza kuwa vifaa hivyo ni juhudi zake za kuwapenda wananchi wake kwa kuhakikisha wanapata mahitaji yao.

Kwa upande wake captain wa timu ya Bungizi fc Mpame Mpame amempongeza diwani huyo kwa kugawa vifaa vya michezo kwenye vitongoji vyote ili kuinua vipaji vya vijana katika kata yake.

Naye katibu wa ccm kata Tengelea Twahili Koki amempongeza diwani huyo kwa kutoa usafiri kwa viongozi wa matawi wote 11 na hivyo kupelekea kutokomeza kabisa hadha ya usafiri kwa watendaji hao wa chama cha mapinduzi.

Hivyo aliongeza kuwa vifaa hivyo vitasomeka ni mali ya ccm na si diwani tena kutokana na jinsi diwani mwenyewe alivyoamua kwa viongozi hao.

Aidha amewataka makatibu tawi wote 11 waliopata baiskeli hizo kuzitunza ili kuhakikisha zi awasaidia kazi za chama kama ilivyokusudiwa kufanyika.