Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Balozi wa Canada nchini Tanzania Bi.Pamela O’Donnell, wakati akiwasili katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma, kufungua Maonesho ya Wiki ya Azaki
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya AZAKI yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia kitabu, wakati akitembelea mabanda, kabla ya kufungua Maonesho ya Wiki ya AZAKI yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma Kutoka kushoto ni Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Vickness Mayao, Mkurugenzi Mtendaji wa Wajibu Ludovick Utouh, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia bidhaa, iliyotengenezwa na Mjasiriamali ambaye ni mlemavu wa macho, Angela Sebastian, wakati akitembelea mabanda, kabla ya kufungua Maonesho ya Wiki ya AZAKI inayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mjasiriamali ambaye ni mlemavu wa macho, Angela Sebastian, wakati akitembelea mabanda, kabla ya kufungua Maonesho ya Wiki ya AZAKI inayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkurugenzi wa Policy Forum, Semkae Kilonzo, kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya AZAKI inayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi,wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya AZAKI inayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Rais wa Foundation for Civil Society, Dkt.Stigmata Tenga, akitoa taarifa kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya AZAKI inayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya AZAKI inayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya AZAKI inayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji ,Foundation for Civil Society (FCS) ,akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya AZAKI inayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Binilith Mahenge ,akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya AZAKI inayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya AZAKI inayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa AZAKI baada ya kufungua Maonesho ya Wiki ya AZAKI inayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
…………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua leo wiki ya Asasi za Kiraia(AZAKI) huku akisema serikali itaendelea kujenga mazingira wezeshi ya utendaji kazi wa AZAKI ili ziweze kushiriki ipasavyo katika agenda ya maendeleo.
Aidha, amezitaka asasi za kiraia kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, mwaka huu.
Akizungumza leo katika uzinduzi wa wiki hiyo iliyoanza leo hadi Novemba 8, mwaka huu,Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali ipo tayari muda wote kushirikiana na AZAKI katika kuleta maendeleo kwenye jamii ya Watanzania.
Amesisitiza AZAKI kuhakikisha zinatekeleza majukumu kwa mujibu wa Sheria.
“Hivyo, hakikisheni mnatekeleza majukumu yenu kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na miongozo iliyopo na mnapotekeleza majukumu yenu hakikisheni mnazingatia misingi ya uwazi na uwajibikaji na katika utekelezaji wa miradi na programu wabainishe vyanzo vyao vya fedha,”amesema.
Waziri Mkuu amewataka kujihusisha na mambo ambayo ni kinyume na Sheria na taratibu za Nchi na badala yake wajikite kwenye mipango, miradi na mikakati kwa kuzingatia vipaumbele vya Taifa.
Kadhalika, amesema serikali itaendelea kuondoa vikwazo vinavyochangia kukwamisha dhamira ya kuboresha maisha ya wananchi na hasa wanyonge huku akiwahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya tano inathamini sana mchango wa Asasi za Kiraia na itaendelea kushirikiana nanyi katika kuboresha maisha ya wananchi wetu hasa wanaoishi maeneo ya vijijini.
Ametoa rai kwa kwa watoa mada na washiriki wa mijadala kwenye maonyesho hayo kuhakikisha wanazingatia maslahi mapana ya Taifa sambamba na kutoa ushauri utakaosaidia kuweka mikakati madhubuti ya kuendeleza Taifa letu kupitia utendaji mzuri wa AZAKI.
Kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, Majaliwa amesema wananchi wengi wamejiandikisha kupiga kura hivyo ni wajibu wa asasi kuhimiza kujitokeza kupiga kura ambapo
wapiga kura 19,681,259 sawa na asilimia 86 ya makadirio ya wapiga kura 22,916,412 wamejiandikisha mwaka huu ikilinganishwa na mwaka 2014 ambao ulifika asilimia 63 ya makadirio.
Ametoa wito kwa watanzania wote wenye sifa kujiandaa kushiriki kupiga kura kwa kuwa ni haki yao kikatiba kwa kuzingatia misingi ya demokrasia na serikali imejipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.
Kwa upande wake Rais wa Foundation for Civil Society, (FCS), Dkt Stigmata Tenga, kupitia wiki ya asasi za kiraia zinapata fursa ya kuonesha shughuli wanazozifanya katika maeneo mbalimbali hapa nchi na kauli mbiu ya wiki hiyo ni “ubia kwa Maendeleo, ushirikiano Kama nguzo ya Maendeleo Nchini Tanzania”.
Ameongeza kuwa hapa nchini kumekuwa na ongezeko la asasi za kiraia zipo takribani elfu 6000 na zimejikita katika maeneo mbalimbali hapa nchini na kujishughulisha na mambo mbalimbali katika kazi za kitaifa, mikoa, wilaya, Tarafa, kata na vijiji” amesema Dkt Stigmata.
Amesema wanashirikiana na Serikali katika majukumu yao, na kwa ushirikiano mkubwa na wanatambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika nyanja mbalimbali kutika kuwatumikia wananchi.
Ameiomba serikali katika bajeti zao waone namna ya kutenga fungu kwa ajili ya asasi za kiraia katika kuziwezesha Kama luzuku kutimiza majukumu yao na kuongeza ufanisi zaidi katika shughuli zao za kila siku kuwatumikia wananchi.
Naye Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema Wizara yake ndio msimamizi Mkuu wa shughuli zote za asasi za kiraia na kunaidara maalumu ambayo inaratibu shughuli zote za asasi za kiraia na wanashirikiana nao vyema.
Ameongeza kuwa ” wanashirikiana vyema na asasi zote za kiraia na asasi nyingi zimejipambanua kufanya kazi na jamii hasa zile za chini kabisa na watu wasiojiweza, katika maswala mbalimbali Kama Afya,elimu,maji na msaada wa kisheria vitu ambavyo vinaungwa mkono na Serikali” amesema Waziri Ummy.