Home Mchanganyiko MHANDISI ATOA HAMASA YA KUSOMA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MITUNDU...

MHANDISI ATOA HAMASA YA KUSOMA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MITUNDU “B” ITIGI SINGIDA

0
 Mdau wa Maendeleo wa Kata ya Mitundu wilayani Itigi mkoani Singida, Mhandisi Felix Dagaki, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mitundu B wakati wa kuchangia harambee ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya shule hiyo iliyofanyika jana.
 Wanafunzi wakiwa kwenye harambee hiyo.
Mdau wa Maendeleo wa Kata ya Mitundu , Mhandisi Felix Dagaki, akizungumza wakati akichangia katika harambee hiyo. Kusho ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe na kulia ni Diwani wa Viti Maalumu (CCM) wa kata hiyo, Rose Madumba.
 Harambee ikiendelea.
 Wanafunzi wakiimba shairi kwenye hafla hiyo.
 
 
 
Na Mwandishi Wetu, Singida
 
 

Mhandisi Felix Dagaki ametoa hamasa kwa wanafunzi kusoma kwa bidii ili waje kuwa viongozi bora hapo baadaye. 
 
Dagaki alitoa rai hiyo wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya  Msingi Mitundu B iliopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida.
 
“Wadogo zangu someni kwa bidii nyie ndio viongozi tunaowategemea baadaye, msiichezee fursa hii mlioipata,pia mjisikie na kuona fahari kusoma katika shule zilizopo maeneo yenu kwani hata mimi najivunia kufika shule niliosoma ya Mitundu ” alisema Dagaki. 
 
Aliongeza kuwa njia pekee ya kuyafikia mafanikio hayo kwa wanafunzi ni kusoma kwa bidii huku wakiwasikiliza na kuwatii walimu wao,hayo yatasababisha wafanikiwe na kuyafikia malengo yao. 
 
Aidha Dagaki alitoa motisha kwa kuwapa fedha waalimu na wanafunzi wa shule hiyo walioshida kusoma, kuandika kuhesabu pamoja na kuchora maarufu kama (KK) ambapo pia katika harambee hiyo alitoa mifuko 20 ya saruji, pamoja na kuchangia shilingi milioni moja kwa ajili ya ujenzi huo. 
 
Hata hivyo aliitaka jamii inayozunguka maeneo ya shule hizo kujenga tabia ya kuchangia ujenzi wa shule ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira tulivu yatakayopelekea kufikia mafanikio.