Home Mchanganyiko TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MABADILIKO MADOGO YA UONGOZI 04 Novemba, 2019 Dar...

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MABADILIKO MADOGO YA UONGOZI 04 Novemba, 2019 Dar es Salaam 

0

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara, Phaustine Martin Kasike amefanya mabadiliko madogo ya Uongozi kwa Mkuu wa Magereza Mkoa Manyara na Msaidizi wa Mkuu wa Kikosi Maalum cha kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM). 

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Parole Makao Makuu ya Magereza Kamishna Msaidizi wa Magereza Lipina Lyimo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Manyara, na aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi Masoud Kimolo amehamishiwa kitengo cha Utawala. 

Aidha, aliyekuwa Mkufunzi wa Mafunzo wa Kikosi Maalum cha Magereza Mrakibu wa Magereza Hamza Abdala amekuwa Mkuu Msaidizi wa Kikosi Maalum. 

Kamishna Jenerali wa Magereza ameeleza kwamba mabadiliko haya yanalenga kuboresha utendaji kazi ndani ya Jeshi la Magereza ili kuongeza ufanisi. 

Alaminoso 

Imetolewa na; SSP – Amina Jumanne Kavirondo 

Msemaji wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara