Home Mchanganyiko ZAIDI YA VYUMBA 16 VYAITAJIKA KWA AJILI YA WANAFUNZI WATAKAOJIUNGA NA KIDATO...

ZAIDI YA VYUMBA 16 VYAITAJIKA KWA AJILI YA WANAFUNZI WATAKAOJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2020 KAGERA

0

Na Silvia Mchuruza,Bukoba

Kufuatia ongezeko la ufuhuru wa wanafunzi katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera zaidi ya wanafunzi 803  sawa na asilimia 39 wanaitaji vyuba 16 vya madarasa ili kuepukana na changamoto ya ukosefu Wa elimu bora.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba Bw,Limbe Moris  wakati akizungumza na wanahabari kuwa manispaa hiyo kwa mwaka 2019 walifaulisha wanafunzi wote 2,074 kujiunga na elimu ya sekondari na kwamba kulingana na ufaulu huo vinahitajika vyumba 64 vya madarasa ya elimu ya msingi kutokana na kuongezeka kwa uandikihwaji Wa wanafunzi Wa darasa la kwanza.

Aidha wakazi wa manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wametakiwa kushiriki katika utatuzi wa changamoto ya vyumba vya madarasa 64 vinavyohitajika kwa ajili wanafunzi wa darasa la kwanza kwa upande Wa elimu ya msingi.

Amesema kuwa jitihada mbalimbali za kukabiliana na changamoto hiyo zinaendelea ambapo tiyari vyumba 18 vimeanza kujengwa kwa fedha za ndani ya halmashauri na kwenye shule 20 za serikali zilizopo manispaa ya Bukoba kila shule inahitajika kuwa na vyumba 2 na kwamba wananchi wajitoe kufanikisha ujenzi huo.

Baadhi ya wakazi manispaa ya Bukoba wamesema kuwa ili kufikia ujenzi wa vyumba hivyo ni lazima ufanyike uhamasishaji wa kutosha kwa jamii kwani wako tiyari kushiriki kwenye ujenzi  Wa madarasa hayo.