Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania( CTI) Bw. Shabir Zavery akizungumza na waandishi wa habari katika semina iliyowashirikisha wanachama wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI) na Wakala wa Usalama na afya mahala pa kazi (OSHA) iliyofanyika kwenye hoteli ya New Afrika jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania( CTI) Bw. Shabir Zavery kulia pamoja na washiriki wengine wa semina hiyo wakifuatilia mada za semina hiyo.
Meneja wa Wakala wa Afya na Usalama mahali pa kazi ‘OSHA’ kanda ya Mashariki Jerome Materu akitoa mada usalama na afya wakati wa semina hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Joyce Mwambungu Mwanasheria Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama mahali pa kazi ‘OSHA’ akifafanua masuala mbalimbali ya kisheria wakati alipotoa mada katika semina hiyo.
Bw. Frank Dafa Mtaalam wa Sera za Biashara (CTI) akichangia hoja katika semina hiyo.
Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakichangia hoja katika semina hiyo.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania( CTI) Bw. Shabir Zavery ameishukuru Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa kutoa elimu kwa wanachama wake kuhusu masuala mbalimbali ya usalama na afya mahali pa kazi.
Bw. Zavery ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika semina iliyowakutanisha wanachama wa Shirikisho na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ilyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Bw. Shabbir Zavery amesema OSHA inafanya kazi kubwa kuhakikisha wafanyakazi wanapotekeleza majukumu yao kazini suala la usalama na afya zao linazingatiwa na kutiliwa mkazo ili kuwe na tija ya kazi viwandani.
Ameongeza kwamba Maofisa wa OSHA wamekuwa wakifanya kazi nzuri kwa kutoa maelekezo na mafunzo badala ya kukomoa hii inatufanya wamiliki wa viwanda kufuata na kuzingatia maelekezo na taratibu zinazotolewa na maofisa kutoka Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA).
Ameongeza kwamba semina hiyo inayotolewa kwa wanachama wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi OSHA ina lengo la kuwapa uelewa wa kutosha wanachama kuhusu Taratibu,Kanuni na Sheria za usalama na afya zinazomlinda mfanyakazi ili kutekeleza majukumu yake kwa tija awapo kazini.
Ameongeza kuwa OSHA imefanya mageuzi makubwa kwa kuondoa baadhi ya tozo zilizokuwa zikikwamisha utekelezaji wa baadhi ya majukumu yetu hivyo kusababisha usumbufu kwa wamiliki wa viwanda tunawashukuru sana Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA)kwa hatua hiyo.
Bw. Shabir ameipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Yanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi zake inazozifanya kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025.