Home Michezo BARUA YANGU KWAKO: TUONDOLEE HIZI KELELE MZEE WANGU

BARUA YANGU KWAKO: TUONDOLEE HIZI KELELE MZEE WANGU

0
Na.Imani Kelvin Mbaga,Dar es Salaam

Kwako mwenyekiti, natumaini kuwa u mzima bukheri wa afya. Pole kwa majukumu mazito ya kuiongoza klabu kongwe kuliko zote zilizopo sasa hapa nchini.
Bila shaka umepata picha ya nini maana ya kuongoza hizi klabu, unaweza ukaingia na heshima yako ukaondoka kwa aibu au kinyume chake.
Huku mtandaoni Mzee wangu kumechafuka, kisa Pyramids. Watu wako walikuwa na uhakika wa kuwatandika Pyramids kwa idadi ya magoli yasiyo pungua matatu. Lakini kama ujuavyo matokeo yakaenda ndivyo sivyo.
Mwajiriwa wako katika benchi la ufundi, Mwinyi Zahera ametajwa mara nyingi zaidi kuliko mtu yeyote, watu hawamtaki tena. Usilipuuzie hili, linaweza kuwa anguko lako baya sana kwakuwa panapokuwa na mgawanyiko km huu uliopo “wanga” hujipenyeza na kuharibu kila kitu.
Hebu basi hima mzee wangu kaeni na kumtoa “kafara” huyu Zahera ili tupumue.
Kwa jinsi hali ilivyo hivi sasa “kimdudu” kimeshang’ang’ania ukivumilia kinaweza kuwa na madhara makubwa mno.
Ndiyo maana ulipounda kamati ya ufundi niliuliza “meno” wanayo, hawa watu wako walinibeza wengine wakasema kwakuwa sijasoma basi sina haki ya kuongea, lakini niliangalia mbali.
Kwakuwa watu wanalalamika bila kujua chanzo, na kwa kawaida yao huwa wakiamua wameamua hebu wape wanachotaka, muondoe Zahera muanze upya, akiondoka watakuwa radhi kwa matokeo yoyote.
Ushauri wangu kwako, najua wewe si muumini wa kuubadilisha mfumo wa uendeshaji wa kkabu, lakini nakuomba pitia upya mtazamo wako na kuzingatia hali halisi iliyopo.
Bado unataka kuendelea kusajili wachezaji kwa kutumia “kubwa kuliko?” (nitakueleza siku nyingine madhara yake)
Unadhani utaweza kushindana na wapinzani wako wa ndani ya nchi na nje kwa kutegemea mapato ya “wiki ya wananchi?” la! Hasha, haiwezekani aslani.
Soka limebadilika sana, siku hizi hadi Kroenke tajiri wa Arsenal na yeye anafungua kibubu, muulize Potch alitaka kutembea na bahati ya msimu uliopita lkn bado mambo hayaendi sawa.
Uchumi ndo kila kitu
Wasaalam