Daktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Henry Mayala akimpima jinsi moyo unavyofanya kazi mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga wakati wachezaji wa timu hiyo walivyofika JKCI jana kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa ya vilabu
Afisa wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Janeth Haule akimpima urefu, uzito, na uwiano wa urefu na uzito (BMI) mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga African Sport Club Clement Mzize wakati wachezaji wa timu hiyo walivyofika JKCI jana kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa ya vilabu