Makamu wa Rais wa Kampuni usambazaji wa pikipiki za miguu mitatu (Bajaji)Sunbeam Auto ltd Kanda ya Mashariki na Kusini Afrika Bw.Denesh Kulkarni akionesha bajaji hiyo mbele ya Wadau mbalimbali waliojitokeza (Hawapo pichani) katika Uzinduzi wa Usafiri wa miguu mitatu maarufu kama Bajaji aina ya Maxima Z zenye uwezo wa kubeba abiria sita pamoja na dereva Jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa Bendi Banana Zoro akitumbuiza katika Uzinduzi wa Usafiri wa miguu mitatu maarufu kama Bajaji aina ya Maxima Z zenye uwezo wa kubeba abiria sita pamoja na dereva Jijini Dar es Salaam.
************************
NA EMMANUEL MBATILO
Kampuni ya inayohusika na usambazaji wa pikipiki za miguu mitatu (Bajaji)Sunbeam Auto ltd ofisi kuu ya Dar es Salaam, imezindua Usafiri wa pikipiki hizo aina ya Maxima Z zenye uwezo wa kubeba abiria sita pamoja na dereva.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo kanda Mashariki na Kusini Afrika Bw.Denesh Kulkarni katika uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza katika Mkutano huo Bw.Kulkarni amesema kuwa wanampango wa kupeleka usafiri huo katika maeneo mbalimbali ili kuweza kurahisisha usafiri katika maeneo ambayo yanauhaba wa usafiri.
Naye Mkurugenzi wa Mauzo wa Kampuni ya Sunbeam Auto ltd Bw. Jestas Kyolike amesema kuwa bajaji ambayo wamezindua inauwezo wa kuhimili kupita katika barabara mbovu zenye changamoto kwa usafiri mwingine kupita kutokana na injini kubwa iliyonayo Bajaji hiyo.
“Ukiangalia bajaji inauwezo kupita katika barabara ambayo ni ndogo kuepukana na foleni za hapa na pale,pamoja inakidhi mazingira hasa jua pamoja na mvua kunyesha uinaweza kumsaidia mtumiaji kutokuwa na usumbufu kama huo utakapojitokeza”. Amesema Bw.Kyolike.