Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang’ata (kulia), akikabidhi kwa Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Laela, Omelina Mgawe, mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Kikundi cha akina mama wauza mboga wa hiyo. Pia altoa msaada wa mabati ya kuezekea soko hilo ili waondokane na adha ya kuuzia bidhaa zao juani.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa (CCM), Bupe Mwakang’ata (kulia),
akikabidhi kwa Diwani wa Kata ya Laela, Sangu, msaada wa mabati 24 kwa ajili ya kuezekea jengo la Soko la Kikundi
cha akina mama wauza mboga wa Kata hiyo, Wilaya ya Sumbawanga Mjini katika hafla iliyofanyika hivi karibuni.
Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang’ata, akizungumza katika mkutano na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Uchile ya Sumbawanga Vijijini . Katika mkutano huo ambao mada kuu ni kupiga vita mimba za utotoni ambapo pia alikabidhi msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang’ata akimkabidhi Mwenyekiti wa Kata ya Mlokola, Teofrida Mbaule msaada wa sh. 500,000,
za kuwawezesha wanawake kibiashara wa kata hiyo. Kata zingine nne zilizopata kiasi kama hicho ni;Kasamsana, Mnokola, Miangalua na Laela B.