Mmoja wa Wadau wa Afya akiuliza swali kwa watoa Mada katika Mkutano wa wataalamu wa afya kutoka katika nchi mbalimbali wakijadili mnyororo wa dawa na vifaa tiba Jijini Dar es Salaam
Mmoja wa Watoa Mada akiwasilisha Mada katika Mkutano wa wataalamu wa afya kutoka katika nchi mbalimbali wakijadili mnyororo wa dawa na vifaa tiba Jijini Dar es Salaam
Wataalamu wa afya kutoka katika nchi mbalimbali Wakifuatilia Mkutano ambao umewakutanisha kukijadili mnyororo wa dawa na vifaa tiba pamoja na changamoto zake uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Mfamasia Mkuu wa Serikali Dkt. Daudi Msasi (Kulia) akiongea na Wanahabari(Hawapo pichani) Kabla ya Mkutano wa wataalamu wa Afya kutoka katika nchi mbalimbali wakijadili mnyororo wa dawa na vifaa tiba kuendelea.
*****************************
NA EMMANUEL MBATILO
Jamii imetakiwa kuacha matumizi holela na yasiyosahihi ya dawa za binadamu ambapo husababisha usugu wa vimelea vya wadudu wa magonjwa katika mwili.
Akizungumza katika mkutano wa wataalamu wa afya kutoka katika nchi mbalimbali wakijadili mnyororo wa dawa na vifaa tiba, Mfamasia Mkuu wa Serikali Dkt. Daudi Msasi amesema kuwa kupunguza kiwango cha dawa ama kuongeza katika dozi husika kunachangia usugu katika miili na hivyo kusababisha dawa kushindwa kufanya kazi pale ugonjwa unapojitokeza tena.
Aidha, Dkt.Msasi amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya maboresho katika ugavi wa dawa na vifaa tiba kwa kuainisha dawa muhimu ambapo zahani ni dawa 30 na hospitali ni dawa 312 huku madaktari wakitakiwa kufuata miongozo iliyopo ya matibabu.
“Dunia inapambana na usugu wa wadudu wa vimelea vya magonjwa yanasosababishwa na dawa na hii inasababishwa na kutumia dawa kiholela aidha chini ya kiwango ama juu ya kiwango”.
Naye Afisa uhusiano wa Shirika la umoja wa Mataifa (UNFPA) Bw.Bright Wallen amesema kuwa UNFPA wamekuwa wakishirikiana na Serikali katika kutoa dawa na vifaa tiba pamoja na kusaidia kutibu watu.
“Takribani wadau 300 wamehudhulia mkutano huu wakijifunza mada mbalimbali zimekuwa zikitolewa na kujifunza na lengo kuu kuona ni namna gani wanaweza kuboresha mfumo wa dawa kwenye masuala ya ugavi”.Amesema Bw. Wallen.
Kwa upande wao baadhi ya wadau waliohudhuria mkutano huo akiwemo Bw. John mvutakamba amesema kuwa mkutano huo utaweza kufanya tathimini ya huduma za afya hususani katika ugavi hivyo kuweza kuanisha changamoto na kuweza kuunda mbinu za kutatua.